Stonek waitangaza Zinazosomwa App: Programu ambayo inakuwezesha kusoma habari zinazovuma na habari za mada uzipendazao kutoka vyanzo maarufu Tanzania

ZInazosomwa App. App moja, vyanzo vingi vya habari. Jua nini kinavuma Tanzania. Pata habari unazopenda kusikia.

Zinazosomwa ni app ambayo inamrahisishia msomaji kupata habari za mada azipendazo na vilevile kujua ni jambo gani linavuma Tanzania

Kazi za app ya Zinazosomwa

  1. Kumkusanyia msomaji habari kutoka vyanzo maarufu zaidi ya  35 Tanzania
  2. Kuzipangilia habari katika mada (mfano Siasa, Burudani, Michezo n.k) na tags za watu au mambo maarufu, kama jambo jipya linalozungumziwa kuhusu nchi, wanasiasa na watu maarufu
  3. Programu au app ya Zinasomwa pia inachambua habari zote zinazofika katika mifumo yake na kugundua ni zipi zinavuma
  4. Inamuwezesha msomaji achague mada anazozipendelea ili iweze kumletea habari hizo kila siku
  5. Inamuwezesha mtu asome habari kutoka kwenye chanzo anachotaka
  6. Inampa msomaji uwezo wa kutafuta habari kwa maudhui, mada, tag au chanzo
  7. Inaonesha ni habari gani zinasomwa sana ndani ya masaa 24
  8. Inampa msomaji uwezo wa kutuma habari kwa ndugu na jamaa kutumia whatsapp, facebook na mitandao mingine

1. trending 2. tag

unga 4. read

3. mada

Dhumuni la App ya Zinazosomwa

“Dhumuni letu kuu ni kumrahisishia msomaji kupata habari kutoka vyanzo mbalimbali na kujua mambo yanayovuma kwa kutumia chanzo kimoja tu, app ya zinazosomwa” Asema Peter Kisinga, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Stonek Limited. Anaoungeza, “Dhumuni jingine ni kuwasadia wamiliki wa vyanzo vya habari kupata wasomaji wengi kupitia app yetu, kwani habari zote zinasomwa kwenye vyanzo husika”

Jinsi ya kuipta App ya Zinasomwa

Kwa sasa app hii inapatikana kwa watumiaji wa simu za Android hapa, itapakana kwenye simu au vyombo vingine baadae.

 

Tovuti ya Zinasomwa

Kwa wale wasio na simu za Android wanaweza kutumia tovuti yetu zinazosomwa, www.zinasomwa.com amabyo inafanya baadhi ya kazi zinazofanywa na app.

Akaunit za Mitandao ya Kijamii ya Zinasomwa

Pia tunawafikia wasomaji kwa kutumia akaunti zetu za facebook (@zinazosomwa) na twitter (@zinazosomwa) ambazo huwa zinaposti habari zinazovuma mara tatu kwa siku.

Related Posts

Write a comment